MFUMO WA SkySchool
Utangulizi SkySchool ni mfumo ambao unalenga kutatua changamoto zote sekta ya elimu, ikiwemo changamoto za walimu, wazazi, utawala, pamoja na wanafunzi kwa kutumia tekinolojia. Mfumo huu unaweza kutumiwa na shule za chekechea, msingi na sekondari. Mfumo huu umeundwa na vipengele vifuatavyo:
  1. Uhifadhi wa taarifa za shule: Kwa kutumia mfumo huu utawala wa shule unaweza kutunza kumbukumbu za taarifa za walimu, wanafunzi pamoja na wafanyakazi wengine yaani wapishi, madereva n.k.
  2. Uhifadhi wa matini ya kufundishia pamoja na mitihani(Online library): Mfumo wa SkySchool unaruhusu matini mbalimbali kuhifadhiwa kama video, documents na mitihani iliyoipita, endapo itahitajika inaweza ikatolewa kama hard copy.
  3. Mawasiliano ya uongozi wa shule na wazazi: Kwa kutumia mfumo huu shule inaweza kutuma ujumbe kwa wazazi wa wanafunzi wote kwa wakati mmoja inapohitaji kutoa taarifa kwa wazazi. Ujumbe huu unamfikia mzazi kweye simu yake ya mkononi ukiwa na jina la shule.
  4. Kufundisha wanafunzi(E-Learning). Mfumo huu unaweza kutumika kufundishia wanafunzi na wakasoma kwa kutumia vishikwambi (Tablets). Mwalimu anaweza kuandaa masomo yake kwa kutumia mfumo na wanafunzi wakayapata kwenye vishikwambi vyao.
  5. Mahudhurio ya wanafunzi: Mfumo unaruhusu kuita na kuhifadhi mahudhurio ya wanafunzi ya kila siku, hii inasaidia shule kufahamu wanafunzi ambao ni watoro shuleni na kuweza kujua athari za wanafunzi watoro shuleni.
  6. Utunzaji na utumaji wa ripoti za kila siku pamoja na kumbukumbu za kifedha, mfumo unaweza kutumika kutunza ripoti za matukio na mambo yanayokuwepo shuleni ya kila siku, pia unaweza kutumika kutunza kumbukumbu za kifedha yaani matumizi ya fedha za shule ya kila siku, matumizi ya fedha katika mradi unaoendeshwa na shule mfano mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Gharama za kutumia Mfumo wa SkySchool. Wasiliana nasi kwa ghalama za msaada zaidi. Wasiliana nasi
TodaySky Technology S.L.P 1552 Dodoma Tanzania Email : management@2daysky.com Phone : +255 787 847 805